Wasichana 82 waliotekwa nyara na Boko Haram wakutana na Rais wa Nigeria

Takriban wasichana 82 wa shule ya wasichana ya Chibok walioachiliwa kutoka umateka wa kundi la Boko Haram wamekutana na rais wa Nigeria Muhamadu Buhari. Walisindikizwa hadi mji wa Abuja na wanajeshi waliokuwa wamejihami kwaA�A�silaha baada ya kukaguliwa naA�A�madaktari. Buhari ambayeA�A�baadaye aliondoka kuelekea Uingereza ili kupokea matibabu, alielezea furaha kufwatia kuachiliwa kwa wasichana hao.

Hatibu wa rais alisema hakuna haja ya raia kuwa na wasi-wasi kuhusu afyaA�A�ya rais kwa kuwa anaenda kufanyiwa uchunguzi waA�A�kawaida wa kimatibabu. Buharu, mwenye umri wa miaka 74 alirejea kutoka Uingereza mwezi wa Machi baada ya kuwa nchini humo kwa wiki saba akipokea matibabu. Hata hivyo ugonjwa anaougua haukubainishwa. Hali yake ya afya ilizua minonga��ono baada ya kukosa kuhudhuiria vikao kadhaa vya baraza la mawaziri.