Washukiwa Wa Ardhi Ya Ubalozi Wa Kenya Mjini Tokyo Waondolewa Mashtaka

Aliyekuwa katibu katika wizara ya mashauri ya nchi za kigeni, Thuita Mwangi na wengine wawili wameondolewa mashtaka kuhusiana na ununuzi wa ardhi ya jengo la ubalozi wa Kenya mjini TokyoA� Japan. Hakimu Kennedy Bidali aliwaondolea mashtaka hayo akisema baadhi ya mashahidi wa upande wa mashtaka kwenye kesi hiyo walishiriki katika utaratibu wa utoaji zabuni ya ununuzi wa ardhi hiyo. Bidali hata hivyo aliamua kwamba mahakama ilishughulikia kilichohitajika kuhusiana na kesi hiyo. Wakili wa upande wa utetezi Paul Muite alisema uamuzi huo ni ishara kwamba tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi pamoja na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma zilifanya uchunguzi duni kuhusiana na swala hilo.A�Muite alisema washtakiwa wangelishtakiwa kwa wizi wa pesa iwapo ulitokea na sio kwa kutozingatia utaratibu wa utoaji zabuni katika wizara hiyo.