Wasafirishaji wa petroli waonywa dhidi ya kuweka vizuizi barabarani

Wafanyibiashara huru wa kusafirisha petroli wametakiwa kukoma kuweka vizuizi katika barabara zinazoelekea kituo cha mafuta za eneo la viwandani jijini Nairobi.

Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet alikuwa amewapa wafaybiashara hao wa usafirisjai mafuta ambao wanalalamikia nyongeza ya ushuru wa asilimia 16 kwa bidhaa za petroli hadi saa kumi na moja jioni kuondoka eneo hilo la sivyo malori yao yanaswe na yeyote atakayepatikana akifunga barabara akamatwe.

Maandamano hao ya wasafirishaji huru wa mafuta yamesababisha zogo la uhaba wa mafuta jijini huku vituo vingi vya petroli vikikosa mafuta na vile vichache vina mafuta vinakumbwa na msongamano wa wandeshaji magari wanaotafuta mauta. Tume ya kuthbiti sekta ya kawi pia imetisishia kuto-toa upya leseni kwa wasafirishaji mafuta ambao walisiriki kwenye maandamano hayo.