Wapinzani nchini Togo waandamana kupinga serikali

Wafwasi wa upinzani nchini Togo wamepuuzilia mbali maagizo ya serikali ya kukomesha harakati za kumtaka rais wa nchi hiyo anga��atuke uongozini.Wanatak+a marekebisho ya katiba kufanywa,ikiwa ni pamoja na kuratibu vipindi viwili tu vya utawala wa urais nchini humo.Wakati ambapo serikali imekubali kufanya mabadiliko ya kikatiba,upinzani umetilia shaka utayari wa serikali kutekeleza marekebisho hayo.Unashuku kuwa huenda rais Faure Gnasingbe atatawala kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja.