Wapalestina wawili wauawa leo kwenye shambulizi karibu na mpaka wa Misri

Wapalestina wawili waliuawa mapema leo asubuhi kwenye shambuliziA�lililotekelezwa na Israeli dhidi ya handaki moja karibu na mpaka wa Misri. Msemaji wa wizara ya afya ya katika utawala wa WapalestinaA�alisema kwenye taarifa kwamba mbali na kuuawa kwa wawili hao, watu wengine watano pia walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo lililotekelezwa na ndege moja ya kijeshi ya Israel. Awali jeshi la Israeli lilikuwa limesema lilitingua makombora kadhaa yaliofyatuliwa na wanamgamboA�kutoka eneo la Sinai nchini Misri dhidi ya mji wake wa Eilat. Hakuna kundi lililodai kufyatua makombora hayo, hatahivyo serikali ya Misri imedai kuwa kundi la Hamas limekuwa likiwasaidia wanamgambo wa Isis katika jangwa la Sinai, madai ambayo yamekanushwa na kundi hilo la Hamas