Wanawake kuwaruhusu kuendesha magari, Saudia Arabia

Vyombo vya serikali nchini Saudia Arabia vimesema kuwa mfalme wa nchi hiyo Salman ametoa agizo la kuwaruhusu wanawake kuendesha magari kwa mara ya kwanzaA� nchini humo.A� Kulingana na idara ya habari ya serikali nchini humo, wizara za serikali zinapaswa kutayarisha ripoti katika muda wa siku 30 na agizo hilo kutekelezwa mnamo mwezi Juni mwaka 2018. Saudi Arabia ni nchi ya kipekee duniani isiyoruhusu wanawake kuendesha magari. Chini ya mfumo wa sasa, ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kupata leseni za kuendesha magari na wanawake wanaoendesha magari hadharani wanakabiliwa na hatari ya kukamatwa na kutozwa faini. Kwasababu ya sheria hiyo, familia nyingi zimelazimika kuwaajiri madereva wa kibinafsi kusaidia kutoa huduma za usafiri kwa jamaa zao wa kike . Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Uingereza, yamefanya kampeini kwa miaka mingi za kutaka wanawake kuruhusiwa kuendesha magari na wengine wamefungwa gerezani kwa kukiuka agizo hilo.