Wanawake Kufaidika Na Mipira Ya Ngono Nchini Ufilipino

Mashirika ya kiserikali nchini Ufilipino yametakiwa kutoa bila gharama mipira ya kufanyia ngono kwa zaidi ya wanawake A�milioni 6 ambao hawana uwezo wa kuinunua.Rais Rodrigo Duterte amesema kuwa amepania kupunguza kiwango cha mimba za mapema,hasa miongoni mwa jamii masikini.Hata hivyo agizo hilo huenda likazua pingamizi kubwa kutoka kwa kanisa la kikatoliki.Mtangulizi wa rais Duterte alijaribu kwa muda mrefu kupitisha mswada A�wa sheria wa A�kuruhusu matumizi ya mipira ya ngono nchini humo,lakini mahakama ya juu kabisa nchini humo ilisimamisha kwa muda usambazaji wa vifaa vya kuwazuia kinamama kushika mimba mnamo mwaka wa 2015 baada ya A�malalamishi kutoka kwa makundi ya kupinga uavyaji mimba.