Wanariadha Ezrah Kiprotich na Polline Wanjiku watawazwa mabingwa wa mwaka huu wa mbio za nusu marathoni
Wanariadha Ezrah Kiprotich Sang na Polline Wanjiku Njeru wa humu nchini walitawazwa mabingwa wa mwaka huu wa mbio za nusu marathoni za Warsaw zilizoandaliwa nchini Poland. Kiprotich, alitumia muda wa saa 1 dakika 01 na sekunde 37 kumshinda Kassa Mekashaw wa Ethiopia aliyemaliza wa pili kwa muda wa saa 1 dakika 01 na sekunde 52 ilihali Hillary Kiptum wa humu nchini alitumia muda wa saa 1 dakika 02 na sekunde 08 kumaliza wa tatu. Kwa upande wa akina dada Polline Wanjiku alitumia muda wa saa 1 dakika 10 na sekunde 01 kuibuka mshindi. Birhan Mhertu Gebrekidan wa Ethiopia alimaliza wa pili mbele ya mwenzake Maeregu Hayelom Shagae aliyetumia muda wa saa 1 dakika 10 na sekunde 52 kumaliza wa tatu.