Wanariadha 29 kuelekea Uhispani kwa mashindano ya ‘masters’

Wanariadha 29 watasafiri kwenda Malaga Uhispania kesho ili kuwakilisha taifa kwenye makala ya pili ya mashindano ya masters yatakayoandaliwa kuanzia tarehe 6 hadi tarehe 16 mwezi huu.

Kikosi cha timu ya Kenya kitanuia kunyakua nishani nyingi za dhahabu baada ya kunyakua tatu katika makala ya mwaka 2016 yaliyoandaliwa jijini Perth Australia. Francis Komu atanuia kutetea taji yake katika mbio za kilomita 21 kwani alinyakua dhahabu mwaka 2016.

Komu aliandikisha muda wa saa 1 dakika 11 sekunde 7 na kumaliza mbele ya Mkenya mwenzake John Birgen aliyeandikisha muda wa saa moja 1 dakika 11 sekunde 20 huku akitwaa nishani ya fedha. Joshua Kipchumba pia alinyakua dhahabu baada ya kuibuka mshindi kwenye mbio za mita elfu kumi.