Wananchi wa Iran washiriki katika upigaji kura

Shughuli ya upigaji kura za urais ilianza leo nchini Iran huku rais Hassan Rouhani akitarajiwa kuwania awamu ya pili.Rouhani mwenye umri wa miaka 68,ambaye ni kiongozi wa kidini mwenye msimamo wa wastani,ambaye aliafikia mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na mataifa yaliostawi mnamo mwaka wa 2015,anapingwa na wawaniaji wengine watatu.Mpinzani wake mkuu Ebrahim Raisi,mwenye umri wa miaka 56,A� ni kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali na ambaye zamani alikuwa kiongozi wa mashtaka na ni mwandani wa kiongozi mkuu wa kiislamu nchini humo Ayatola Ali khamenei.Ikiwa hakuna mwaniaji atakayejipatia asslimia 50 ya kura katika awamu ya kwanza,kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi huo juma lijalo.Tangu mwaka wa 1985 ,rais aliye mamlakani amekuwa akichaguliwa na raia kwaA� kipindi cha pili,huku ikizingatiwa kuwaA� Ayatola Khamnei mwenyewe alishinda awamu ya pili ya uongozi.Takriban raiaA� milioni 54 wamesajiliwa kuwa wapiga kura.Kwa mujibu wa wizara ya mashauri ya ndani takriban vituo 63,500 vya kupigia kura ambavyo vilifunguliwa m,wendo wa saa mbili asubuhi za za Iran.Kwenye chaguzi zilizopita muda waA� kupiga kura umeongezwa kutokana na idadi ya watu iliojitokeza kupiga kura.