Wanamgambo 89 Wa Boko Haram Wahukumiwa Kunyongwa Nchini Cameroon

Cameroon  imewahukumu kunyongwa  wanamgambo 89 wa kundi la kigaidi la Nigeria la Boko Haram.Wanamgambo hao walipatikana na hatia ya kutekeleza ukatili na mahakama ya kijeshi ya Cameroon kutokana na kuhusika kwao katika mashambulizi  kadhaa ya kigaidi kaskazini mwa nchi hiyo kwenye mpaka Cameroon na Nigeria.Cameroon ilipitisha sheria za kukabiliana na ugaidi mnamo mwaka wa 2014 ambao adhabu yake ni kifo.Waathiriwa hao 89 ni kati ya wanamgambo 850 waliotiwa nguvuni nchini humo na kuhusishwa na kundi la Boko Haram.Kufuatia kubuniwa kwa sheria hizo,shirika moja la kutetea haki za binadamu  limetaka sheria za Cameroon kufanyiwa marekebisho.Mamia ya watu wameuliwa kwenye visa tofauti vya mashambulizi ya kigaidi nchini Cameroon tangu ilipochangia kikosi cha  jeshi la kanda hiyo la kukabiliana na ugaidi mwaka jana.