Wanajeshi watano kutoka Sudan wauawa na waasi Yemen

Wanajeshi watano wa Sudan wameuawa kwenye mapigano dhidi ya waasi wa kabila la Houthi nchini Yemen. Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Sudan, si jambo la kawaida kukiri kuwapoteza wanajeshi wa Sudan tangu nchi hiyo ilipowapeleka mamia ya wanajeshi wake nchini Yemen mwaka 2015. Haya hivyo jeshi hili halikusema ni lini wanajeshi hao waliuawa. Hatibu wa jeshi la Sudan, Brigedia Jenerali Ahmed Khalifa al-Shami amesema waliwapoteza wanajeshi watano na wengine-22 kujeruhiwa. Vita hivyo vilivyodumu kwa miaka miwili vinahusisha waasi wa kabila la Houthi na wanajeshi wa serikali ya Rais Abd-Rabbu Mansour Hadi wa Yemen, wanaoungwa mkono na Kuwait, Qatar, Milki za Kiarabu, Misri, Jordan na Morroco.

A�