Wanajeshi wa Syria walaumiwa kwa kutumia silaha za kemikali kwa binadamu

Majeshi ya Syria yametumia silaha za kemikali mara nne tangu mwezi wa Disemba mwaka jana, zikiwemo ziliowauwa takriban watu 100, kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch. Nukuu za ripoti ya shirika hilo zilisema kuwaA� ukiukaji huo wa haki za binadamu umekuwa mtindo kwa uongozi wa taifa la Syria na kuwa visa hivyo vinaweza kuhesabiwa kuwa uhalifu dhidi ya binadamu. Majeshi ya Syria yameimarisha utumizi wa kemikali ya klorini,mbali na kutumia makombora yaliotiwa gesi ya klorini dhidi ya rais wa kaswaida hasa karibu na mji wa Damascus.Ripoti hiyo itachapishwa rasmi siku ya jumatatu.