Wanajeshi Wa Marekani Washambulia Kambi Ya Al-Shabab

Wanajeshi wa Marekani,walishirikiana na wenzao wa Somalia kwenyeA� shambulizi dhidi ya kambi ya mafunzo ya wanamgambo wa Al- Shabab siku ya jumatano.Wanamgambo kadhaa wa kundi hilo waliuliwa kwenyeA� shambulizi hilo.Awali kundi hilo lilidai kuwa A�lilipinga shambulizi hilo la wanajeshi wa kigeni,lakini maafisa wa kijeshi wa Marekani walipinga dai hilo na kusema wanamgambo kadhaa waliuliwa kwenye shambulizi hilo.Shambulizi hilo lilitokea baada ya jingine lililotekelezwa na walinda usalama wa Marekani dhidi ya kambi ya kutoa mafunzoA� kwa magaidi siku ya jumamosi.Wafwasi wa Al-Shabab walidai kuwa ni mpiganaji wao mmoja tu aliyeuliwa kwenye mapigano hayo,lakini idara ya ujasusi ya Somalia ilisema kuwaA� takriban wanamgambo 15 wa Al Shabab waliuliwa kwenye mtafaruku huo.Aidha idara hiyo ilisema shambulizi hilo lilimlenga kiongozi mashuhuri wa Al Shabab ,ambaye aliuliwa kwenyeA� mapigano hayo.Ujumbe wa muungano wa Afrika nchini Somalia haujasema lolote kuhusu tukio hilo.