Wanajeshi wa KDF wasaka Al-shabaab Lamu

Afisa mkuu wa polisi wa eneo la Pwani Larry Kienga�� amesema ndege za helikopta za vikosi vya ulinzi vya Kenya zinafanya doria katika sehemu ya Nyongoro kaunti ya Lamu huku maafisa wa usalama wakiwasaka wauaji wa polisi wawili wa utawala. Kienga�� alisema maafisa hao walishaumbiliwa na kuuawa na wengine watatu wakajeruhiwa baada ya wanamgambo wa Al-Shabaab kushambulia gari la kusindikiza msafara walilokuwa wakisafiria huko Nyongoro, kwenye ya Lamu-Malindi. Aliongeza kwamba maafisa hao waliokuwa wakisindikiza mabasi matano ya abiria kutoka Lamu hadi Mombasa,walifariki papo hapo. Gari la maafisa hao lilibaki nyuma baada ya basi moja lililokuwa limesimamishwa na wanamgambo waliokuwa na silaha kwenda taratibu. Washambuliaji waliokuwa wamevalia mavazi ya kijeshi waligawa vijikaratasi kwa abiria lakini hawakuwadhuru.