Wanahabari watahadharishwa dhidi ya taarifa za uwongo

 

Wanahabari wametahadharishwa dhidi ya kutoa taarifa za uongo kwa kusambaza kupitia mtandao wa tweeter taarifa kutoka kwa vyanzio visivyojulikana wala kuaminika. Afisa mkuu mtendaji wa Baraza la vyombo vya habari nchini David Omwoyo alisema wanahabari wanapaswa kujaribu kutafuta habari za kuaminika kutoka kwa vyanzo vya kuaminika. Akiongea wakati wa mkutano wa kuwahamasisha wanahabari kuhusu jinsi ya kushughulikia taarifa kabla ya kuzisambaza kwenye vyombo vya habari, Omwoyo alisema kwamba picha zinazowekwa kwenye mitandao pia zinaweza kuwa chanzo cha taarifa za uongo kwa vile watu hubadili picha hizo kwenye mitandao na kutangaza habari za uongo.

Mkuu wa kitengo cha kuangalia taarifa kwenye baraza la vyombo vya habari nchini, Leo Mutisya alisema wamepata mfumo unaoweza kupata, kutoa na kunakili habari za matamshi ya chuki kwenye televisheni, magazeti, redio na mitandao ya kijamii. Aliongeza kwamba visa viwili vya matamshi ya chuki vimeripotiwa katika kituo cha Kameme Fm, na wakataja vyanzo vya habari za uongo kuwaA´┐Ż theeveningpost.co.ke, kahawatungu, na wengineo. Meneja wa vipindi wa baraza hilo la vyombo vya habari Victor Bwire aliwahimiza wanahabari kuchunguza jinsi ya kushughulikia teknolojia yakiwemo maadili ya kikazi na kuwa wanahabari wenye utaalamu.