Wanafunzi zaidi ya 900,000 kufanya mtihani wa darasa la nane

Zaidi ya wanafunzi 900,000 wanatarajiwa kufanya mtihani wa darasa la nane mwaka huu. Mtihani huo ulioanza leo huku kukiwa na mabadiliko makubwa kwenye usimamizi wake utakamilika Alhamisi.

Hatua hizo zilitangazwa na waziri wa elimu Dr Fred Matianga��i kwa lengo la kukabiliana na visa vya udanganyifu vilivyothihirika mwaka uliopita. Kwenye shule ya msingi ya Aga Khan jijini Nairobi, wanafunzi tuliozungumza nao walieleza matumaini ya kupata matokeo mazuri kwenye mtihani huo. Na katika shule ya msingi ya Nairobi, mwalimu mkuu Kanyingi Machira aliwahimiza wanafunzi kutojihusisha na visa vya udanganyifu.

Walimu kwa upande wao wanasema wamewaandaa vyema wanafunzi na wanatarajia matokeo mazuri. Barala la kitaifa la mitihani linasema hatua madhubuti zimechukuliwa kuimarisha usalama na kuhakikisha mtihani huo unaendelea bila changamoto zozote.

A�

A�