Wanafunzi Wateketeza Mali Ya Mamilioni Ya Pesa Katika Shule Ya Itierio Kisii

Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa jana usiku iliharibiwa baada ya wanafunzi wa shule ya upili ua wavulana ya Itierio iliyoko kaunti ya Kisii kuteketeza shule yao.Wanafunzi hao waliteketeza madarasa kadhaa , mabweni saba na ofisi kadhaa. Vurugu zilianza wakati wanafunzi hao waliponyimwa ruhusa ya kutazama mechi za kombe la Euro 2016 zinazoendelea nchini Ufaransa.Mwalimu mkuu wa shule hiyo Andrew Otara amesema wanafunzi hao waliteketeza mabweni hayo na kuvunja vioo vya madirisha muda mfupi baada ya kumalizika kwa muda wa burudani la jioni. Kamishna wa kaunti hiyo, Kula Hache, ameshutumu kisa hicho akisema uchunguzi umeanzishwa ili kuwachukulia hatua waliohusika na uteketezaji huo.

Gavana wa kaunti ya Kisii, James Ongwae, amesema ameshangazwa na kisa hicho akisema wadau wa elimu wanafaa kutafuta mbinu za kuzuia visa kama hivyo.

Hivi majuzi shule saba katika kaunti ya Kericho, Tengecha Boys, Londiani Boysa��, Cheptenye Boysa��, Chepsir Boysa��, Kericho High , Kabianga Boysa�� naA� Chumo Boysa�� ziliteketezwa na wanafunzi.Shule ya Kaplong Boys High katika kaunty jirani ya Bomet pia iliteketezwa alhamisi usiku karibu mwezi mmoja baada ya bweni la shule ya Longisa Boys katika kaunti hiyo kuteketezwa.Wanafunzi wa shile nyingine kadhaa kote nchini wamefanya ghasia na kuteketezwa shule zao siku za hivi majuzi.