Wanafunzi watatu wafariki kwenye ajali ya barabara

Wanafunzi watatu kutoka kaunti ya Turkana walipoteza maisha yao leo asubuhi na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati basi la shule ya upili ya Lokichar walilokuwa wakisafiria kubingiria mara kadhaa kwenye eneo la mteremko huko Kaptimbor kwenye barabara ya Kabarnet-Iten. Wanafunzi hao walikuwa wakirejea shuleni mapema leo asubuhi baada ya kushiriki kwenye michezo katika shule ya upili ya Kabarnet. Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi kaunti ya Baringo, Peter Ndung’u alisema ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa moja asubuhi. Haijabainika ni wanafunzi wangapi walikuwa kwenye basi hilo. Miili ya wanafunzi waliofariki imepelekwa katika chumba cha maiti cha hospitali kuu ya wilaya mjini Kabarnet huku majeruhi wakitibiwa hospitalini humo.