Wanafunzi Wanane Wa Shule Ya Upili Ya Sunshine Washtakiwa Kupanga Njama Ya Kutekeleza Uhalifu

Wanafunzi wanane wa shule ya upili ya Sunshine wameshtakiwa kwa kupanga njama ya kutekeleza uhalifu na kujaribu kuchoma mali ya shule. Wanafunzi hao walikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu wa mahakama ya watotoA´┐ŻLucy Gitaru. Upande wa mashtaka ulisema wanafunzi hao walipanga njama ya kuchoma bweni kwa jina Marsabit shuleni humo mnamo tarehe 22 mwezi Julai mwaka huu. Hakimu huyo atatoa uamuzi leo alasiri kuhusu iwapo masharti ya awali ya kuwaachilia wanafunzi hao kwa dhamana ya shilingi elfu-50 yatabadilishwa. Hii ni baada ya upande wa mashtaka kutoa kupendekeza dhamana hiyo iongezwe kwa shilingi elfu-20 pesa taslimu kila mmoja kusubiri kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi hiyo.