Wanafunzi wa kike na walimu wao waponea shambulizi lililotekelezwa na Boko Haram

Wanafunzi wa kike pamoja na walimu katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wameponea shambulizi dhidi ya shule moja ya mabweni lililotekelezwa na wanamgambo waA� Boko Haram . Hii ni kulingana na walioshuhudia tukio hilo. Walisema kuwa wanamgambo hao waliokuwa kwenyeA� malori waliwasili katika mji wa A�Dapchi, katika jimbo laA� Yobe siku ya Jumatatu usiku na kuanza kufyatua risasi na kurusha vilipuzi. Walimu na wanafunzi walioshtushwa na vurumai hiyo, walikimbilia usalama wao . Wakazi katika mji huo wanasema kuwa wanamgambo hao walikuwa wamepanga kuwateka nyara wanafunzi hao wa kike kutoka mji waoA� . Wanamgambo hao walipokosa mtu katika shule hiyo, walipora majengo hayo. Walioshuhudia waliongeza kuwa baadaye vikosi vya usalama vya Nigeria vikisaidiwa na ndege za kijeshi waliweza kukabiliana na shambulizi hilo. Mnamo mwezi Aprili mwakaA� 2014, Kundi la wanamgmbo la Boko Haram liliwateka nyara zaidi ya wasichanaA� 270 kutoka shule moja katika mji wa Chibok ulioko Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo . Mwezi Septemba mwaka jana, zaidi ya wasichana hao walijiunga tena na familia zao katika sherehe iliyoandaliwa katika mji mkuu wa Abuja