Wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi waandamana kushinikiza kuwachiliwa huru kwa Babu Owino

Mapema jana, wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi walikabiliana na polisi huku wakishinikiza kuwachiliwa huru kwa mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino. Polisi walilazimika kutumia vitoza machozi kuwatawanywa wanafunzi ambao walikuwa wamefunga barabara ya State House na kuwalazimisha wenye magari kutumia barabara mbadala. Hata hivyo kiongozi wa wanafunzi Samuel Ragira amejitenga na maandamano hayo akisema kuwa wale wanaoandamana wamelipwa na baadhi ya wanasiasa. Alitoa wito kwa wanasiasa kukoma kuwaingiza wanafunzi katika siasa zisizofaa bila kuzingatia masomo yao.A� Ragira alitoa wito kwa wanafunzi kusalia watulivu na kumuacha mbunge huyo wa Embakasi mashariki kukabiliana kwa njia ifaayo na kesi hizo zinazomkabili mahakamani.