Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Nairobi Waandamana Kupinga Kuchaguliwa Kwa Babu Owino

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi walifanya maandamano leo asubuhi kupinga kuchaguliwa tena kwa Babu Owino kuwa mwenyekiti wa chama cha wanafunzi chuoni humo kwa hatamu ya nne. Wanafunzi hao walifunga barabara kuu ya Uhuru na kulazimu wenye magari kutumia njia mbadala. Wanafunzi hao walikabiliana na polisi kwa muda wa dakika-30 kabla ya hali ya utulivu kurejeshwa. Wanafunzi hao wamekuwa wakiandamana tangu siku ya Jumamosi baada ya Owino kuibuka mshindi kwenye uchaguzi huo ambao wasimamizi wa chuo kikuu cha Nairobi walisema ulikuwa halali. Baadhi ya wanafunzi walisema kulikuwa na visa vya udanganyifu kwenye uchaguzi huo ambapo Owino alipata zaidi ya kura elfu-18 dhidi ya mpinzani wake Mike Jacob aliyepata kura elfu-3. Wanafunzi hao walizua vurugu wakishinikiza kutimuliwa kwa Owino ambaye tayari alikuwa ameapishwa