Wanafunzi Wa Chuo Kikuu cha Cooperative Wahusika Kwenye Ajali

Wanafunzi wawili kutoka chuo cha Cooperative University College huko Karen yahofiwa wamefariki baada ya matatu waliyokuwa wakisafiria kuacha barabara na kupinduka.
Kundi la zaidi ya wanafunzi 30 wanauguza majeraha mabaya kufuatia ajali hiyo mbaya. Wanafunzi hao walikuwa wakiandaa kufanya kampeini kabla ya uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi.
Mkuu wa chuo hicho Douglas Shitanda alisema kwamba waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali mbali mbali miongoni mwao zikiwemo hospitali ya Karen, Coptic na Kenyatta kwa matibabu. Basi lao lilipoteza mwelekeo baada ya wanafunzi wengi kuninga��inia upande mmoja wa basi hilo.