Wanafunzi kupokea vitabu vya kusoma kutoka kwa serikali mwaka ujao

Waziri wa elimu Dkt. Fred Matiang’I ametangaza kuwa wanafunzi wataanza kupokea vitabu vya kusoma moja kwa moja kutoka kwa serikali kuanzia januari mwaka ujao. Matiang’I amesema sera hii mpya itahakikisha kila mwanafunzi anapata kitabbu cha kusoma kwa mgao wa 1:1 kwa kila mwanafunzi katika shule zote za umma. Akiongea katika sherehe za kukabithi shirika la kuchapisha vitabu cha KLB, cheti cha ubora cha dunia ISO , jijini Nairobi, waziri huyo amesema sera hiyo mpya inatarajiwa kuwazuia matapeli wanaoungana na wakuu wa shule ili kusambaza vitabu vya kusoma ambavyo havijaidhinishwa na wizara ya elimu kwa bei ya juu. Waziri Matianga��I, amesema sera hii mpya ni afueni kwa wachapishaji kwani serikali itanunua vitabu vya kusoma moja kwa moja kutoka kwao . waziri huyo pia aliongeza kuwa usambazaji wa vitabu hivyo utafanywa kwa wakati ufao kando na ilivyokuwa hapo awali ambapo jukumu hilo liliachiwa wakuu wa shule.