Wanafunzi-7 Nyahururu Wafikishwa Mahakamani Kwa Kupanga Kuteketeza Bweni La Shule

Wanafunzi-7 wameshtakiwa katika mahakama ya Nyahururu kwa uharibifu na kupanga kuteketeza bweni la shule. Wavulana hao wawili wa shule ya upili ya Irigithathi katika kaunti ya Nyandarua, walikanusha mashtaka ya kuteketeza bweni la mbao usiku wa tarehe 30 mwezi Julai mwaka huu katika shule hiyo. Hakimu mkuu mkazi, Charo Momanyi aliwaachilia kwa dhamana ya shilingi elfu-150 pesa taslimu kila mmoja na mdhamana wa shilingi elfu-70 pesa taslimu. Wanafunzi wengine watano wa shule ya upili ya Ngai Ndeithia katika kaunti hiyo, walikanusha mashtaka ya kupanga kuteketeza bweni lao. Wavulana hao wawili na wasichana watatu walikamatwa katika kijiji cha Shauri wakiwa na petroli iliyokuwa katika chupa ya lita moja. Hata hivyo walipewa dhamana ya shilingi laki-1 pesa taslimu kila mmoja. Kesi hizo mbili zitasikizwa tarehe 29 mwezi huu wanafunzi hao watakapoenda likizo