Chuo Kikuu Cha Nairobi Chatimua Wanafunzi 62 Kwa Kusababisha Ghasia

Chuo kikuu cha Nairobi kimewaagiza wanafunzi 62 kuondoka chuoni kutokana na ghasia na uharibifu wa mali ulioshuhudiwa kwenye chuo kikuu hicho wiki mbili zilizopita.A�A� Mike Jacobs aliyepinga uchaguzi ni miongoni mwa wanafunzi walioagizwa kuchukua barua zao za kutakiwa kundoka chuoni kutoka kwa msajili wa wanafunzi kufikia Ijumaa wiki hii. Chuo kikuu hicho kilifungwa kwa muda usiojulikana wiki iliyopita baada ya wanafunzi kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa chama chao cha SONU, ambapo Babu Owino alitangazwa mshindi. Jacobs aliibuka katika nafasi ya nne kwenye uchaguzi huo. Wanafunzi wengine ni pamoja na Harold Mugozi aliyekuwa akiwania kiti cha katibu mkuu , Robert Choro na Teresa Wanja. Wanafaunzi hao walichoma afisi za chama cha Sonu na mabweni wakati wa maandamano hayo. Naibu chansela Prof. Peter Mbithi ametoa tangazo kupitia magazeti ya humu kuhusu hatua hiyo,pamoja na majina ya wale walioagizwa kuondoka chuoni. Amesema chuo kikuu hicho kimechukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanafunzi 62 kwa kushiriki kwenye maandamano na uharibifu wa mali.