Wanachama Wa LSK Wafanya Uchaguzi

Uchaguzi wa chama cha wanasheria hapa nchini unaendelea kwa sasa huku mawakili watatu wakigombea wadhifa wa mwenyekiti wa chama hicho kuchukua mahala pa Eric Mutua ambaye hatamu yake ilitamatika leo.A�Wagombeaji hao ni pamoja na aliyekuwa rais wa chama cha wanasheria kanda ya Afrika Mashariki,A� James Aggrey Mwamu, mwanachama wa sasa wa baraza kuu la LSK,A� Allen Gichuhi na wakili Isaac Edward Okero. Mbali na uchaguzi wa mwenyekiti, mawakili hao 7,154 watamchagua mwakilishi wao kwenye tume ya kuajiri maafisa wa idara ya mahakama huku hatamu ya Florence Mwangangi ikimalziika leo. Wanaowania wadhifa huo ni Mercy Deche, Jane Abuodha, Mary Karen Soroboit na njeri Onyango. Jeniffer Shamalla naA� Faith Waigwa wanagombea wadhifa wa naibu mwenyekiti wa LSK kuchukua mahala pa Renee Omondi. Uchaguzi huo unasimamiwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka na unatekelezwa katika vituo-25 vya kupigia kura vilivyoko katika mahakama mbali mbali kote nchini. Jijini Nairobi uchaguzi huo unaendelea katika mahakama za Milimani huku kituo kikuu cha kuhesabia kura kikiwa kwenye makao makuu ya chama cha LSK mtaani Lavington.