Wamalwa awahimiza magavana kutenga ardhi kwa ujenzi wa mabwawa ya maji katika kaunti zao

Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa amewahimiza magavana kutenga ardhi kwa ujenzi wa mabwawa ya maji katika kaunti zao.Akiongea katika kijiji cha Arsin kaunti ndogo ya Samburu kaskazini,waziri huyo alisema kuwa ujenzi wa mabwawa hayo utaigharimu serikali zaidi ya shilingi bilioni 30 na utasaidia katika kuhifadhi maji ya mvua kwa matumizi ya nyumbani na mifugo.A�Wamalwa aliongeza kuwa serikali ya kitaifa ilafadhili ujenzi wa bwawa moja kubwa katika kaunti zote 47 kama hatua ya kukabiliana na ukame na pia kutumika katika shughuli za kilimo kama sehemu ya ajenda nne mkuu za kimaendeleo za A�serikali. Wamalwa alisema tayari mabwawa yameaza kujengwa katika baadhi ya kaunti na akawataka magavana kutenga ardhi ya ujenzi huo.