Wamalwa ahimiza ushirikiano baina ya Serikali ya Kitaifa na Kaunti

Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa ameihimiza serikali ya kitaifa na zile za kaunti kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuwawezesha Wakenya kupata manufaa kamili ya ugatuzi.Alisema mizozo ya kila mara kati ya ngazi hizo mbili za serikali inahujumu utoaji huduma kwa wananchi.Kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake,na katibu msimamizi Hussein Dado hukoA�A�Nyeri wakati wa warsha kuhusu mbinu mbadala ya utatuzi wa mizozo,Wamalwa alisema ni jambo la kusikitisha kwamba pesa nyingi za umma zinatumika kusuluhisha mizozo mahakamani badala ya kutekeleza miradi ya maendeleo.