Walofanya vizuri kwenye mtihani wa KCPE wazidi kupongenzwa

Gavana wa kaunti ya Meru Kiraitu Murungi amewapa pongezi wanafunzi pamoja na walimu katika shule za msingi kwenye kaunti hiyo kwa matokeo mazuri kwenye mtihani wa kitaifa wa (K.C.P.E). Kiraitu ametaja  matokeo kuwa ya kuridhisha ikilinganishwa na miaka iliyopita .Aidha amemshukuru  waziri wa elimu Dr. Fred Matiang’i kwa kuweka mikakati kuhakikisha kuzuia  visa vya  udanganyifu wakati wa mtihani huo.Kauli sawa na ya gavana huyo imetolewa na kamishna wa kaunti hiyo  Wilfred Nyangwanga, ambaye ameahadi kufanya kila juhudi kuhakikisha hakuna visa vya udanganyifu vinatokea wakati wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne -K.C.S.E unaoendelea. Wawili hao walikuwa wakiongea katika hafla iliyoandaliwa kuwapongeza wanafunzi na shule zilizofanya vyema kwenye mtihani wa kitaifa wa K.C.P.E mwaka huu.