Walipuaji Mabomu Ya Kujitoa Mhanga Waua Watu 30 Iraq, Huku Idadi Ya Waliofariki Katika Shambulizi lingine Baghdad Ikiongezeka Kutoka 250 hadi 292

Walipuaji mabomu wa kujitoa mhanga na wapiganaji wamewaua takriban watu 30 kwenye madhabahu ya Kishia nchini Iraq, katika shambulizi ambalo kundi la Islamic State limedai kutekeleza. Shambulizi hilo lilianza wakati mwanamme mmoja alipolipua vilipuzi kwenye lango la kaburi la Sayid Mohammed bin Ali al-Hadi,mjini A�Balad. Wapiganaji hao waliingia kwenye eneo hilo na kuwafyatulia risasi waumini. Wakati huo huo idadi ya watu waliofariki kufuatia shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililotekelezwa siku ya Jumapili jijini Baghdad imeongezeka kutoka 250 hadi 292. A�Shambulizi hilo lililenga kituo cha kibiashara katika eneo la Karrada lenye washia wengi jijini humo. Kundi la Islamic State lilidai kuhusika kweney shambulizi hilo baya zaidi nchini humo tangu uvamizi ulioongozwa na marekani mwaka 2003. Kundi hilo hufuata kanuni kali za dhehebu la Kiislamu la Sunni na mara nyingi huwalenga Washia ambao linawachukulia kuwa waasi.