Waliosajiliwa Zaidi Ya Mara Moja Waonywa

Serikali leo asubuhi ilianzisha harakati za kuwaondoa katika sajili ya kitaifa watu ambao wamesajiliwa zaidi ya mara moja. Kulingana na waziri wa usalama, Joseph Nkaissery shughuli hiyo itamalizika tarehe 31 mwezi huu.A� A�Nkaissery alitoa wito kwa wale ambao wameathiriwa kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika shughuli hiyo, akionya kwamba wale ambao hawatafanya hivyo watakamatwa na kushtakiwa. Waziri huyo aliwaagiza wakenya wanaoishi nje ya kambi ya wakimbizi ya Daadab kushughulikiwa katika afisi ya naibu wa kamishna aliye karibu na wale wanaoishi ndani ya kambi hiyo kwenda kwa afisi ya naibu wa kamishna ili kambini humo. Alisema waathiriwa wanapaswa kubeba nakala ya kitambulisho au stakabadhi zao za usajili. A�Visa vya kusajiliwa zaidi ya moja moja vinahusisha wakimbizi ambao wamejiandikisha kuwa wakenya, na pia wakenya ambao wamejiandikisha kuwa wakimbizi. A�