Waliopata Alama 400 Na Zaidi Kujiunga Na shule Za Kitaifa

Watahiniwa wapatao 24,795 wa mtihani wa darasa la nane KCPE wamechaguliwa kujiunga na shule 103 za kitaifa.Waziri wa elimu alisema jana kwamba watahiniwa wote waliopata alama 400 na zaidi wamechaguliwa kujiunga na shule za kitaifa ambazo walichagua.Aidha waziri alisema watahiniwa tano bora wa kike na kiume kutoka kila wilaya wamechaguliwa kujiunga na shule za kitaifa kwa kuzingatia uchaguzi wao wakati wa kujisajilisha kwa mtihani.Akiongea katika taasisi ya ustawishaji mtaala wa masomo jijini Nairobi,Dr. Matiana��gi alisema uchaguzi wa wanafunzi watakojiunga na shule za kaunti na zile za kaunti ndogo utafanywa tarehe 15 na 19 mwezi huu.Waziri pia alitangaza kuwa wanafunzi waliochaguliwa watahitajika kufika shuleni kati ya tarehe 9 na 16A� mwezi januari.