Walimu watatu wakamatwa kwa madai ya uwindaji haramu Msumbiji

Upande wa mashtaka nchini Msumbiji umesema kuwa Walimu watatu wamekamatwa kwa madai ya kujihusisha katika uwindaji haramu wa pembe za ndovu . Carolina Azarias alizitaja habari hizo kuwa za kuhofisha kwa sababu wawindaji hao haramu huenda wakawahusisha wanafunzi wao katika kitendo hicho haramu. Alisema kuwa watatu hao pamoja na afisa mmoja wa idara ya misitu wamezuiliwa katika mji wa Beira baada ya kupatikana na pembe hizo za ndovu na mawe ya thamani.