Walimu wakuu na manaibu wao shule za sekondari watakiwa kuwa shahada ya uzamili

Tume ya kuwaajiri walimu nchini ,TSC imesema walimu wakuu wa shule za sekondari na manaibu wao kuanzia mwaka ujao watahitajika kuwa na shahada ya uzamili katika elimu.Afisa mkuu wa tume ta TSC,Dr. Nancy Macharia,amesema walimu wakuu wa shule za msingi na manaibu wao watahitajika kuwa na shahada ya digree katika elimu.Akiongea jijini Mombasa wakati wa mkutano wa walimu wakuu wa shule Dr. Macharia aliwahimiza walimu wakuu elfu kumi na mbili wanaohudhuria mkutano huo kukubali mabadiliko hayo ya sera.Miongoni mwa mabadiliko hayo, Dakt. Macharia alisema ni pamoja na agizo kwamba walimu wakuu wa shule za msingi, za secondary na vyuo hawataruhusiwa kuhudumu katika kaunty zao za nyumbani au kuhudumu katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka tisa.