Walimu Nigeria wafeli mtihani wa wanafunzi

Maelfu ya walimu wa shule za msingi katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kaduna wanatarajiwa kufutwa kazi baada ya kufeli mtihani uliokuwa umetungiwa wanafunzi wao wa umri wa miaka sita. Gavana wa jimbo hilo Nasir El-Rufai amesema kuwa walimu elfu 21,780 ambao ni thuluthi mbili ya walimu hiyo walikosa kufikisha asilimia 75. Alisema kuwa walimu wapya elfu 25 wataajiriwa kuchukuwa nafasi zao. El-Rufai alisema kuwa swala la idadi ya wanafunzi kwa walimu litashughulikiwa. Alisema baadhi ya maeneo yana mwalimu mmoja kwa wanafunzi tisa huku mengine yakiwa na mwalimu mmoja anayefunza wanafunzi mia moja. A�