Walimu kupewa mafunzo kabla ya mtaala mpya wa masomo mwakani

Tume ya kuwaajiri walimu nchini (TSC) imesema walimu wote watapewa mafunzi ya kutosha kabla ya kuanza kwa mtaala mpya wa masomo mwakani. Akiongea huko Mombasa kwenye mkutano wa 13 wa chama cha walimu wakuu wa shule za msingi (KEPSHA), Afisa mkuu mtendaji wa tume ya TSC Nancy Macharia alisema walimu wakuu watatekeleza jukumu-ongozi katika kuangalia utekelezaji wa mtaala huo. Macharia alisema mtaala huo mpya wa 2-6-3-3 unanuia kuufanya mfumo wa shule kuwa wa vitendo zaidi kwa kuwapa wanafunzo ujuzi ili kuwasaidia kujiendeleza kimaisha. Hali isiyojulikana kuhusu hatima ya mitihani ya kitaifa imewafanya walimu wengi kutafuta ufafanuzi kuhusu swala hilo huku baadhi wakitaka kujua jinsi wanafunzi watakavyotathminiwa bila kudhuru ubora wa elimu.

Naibu mkurugenzi mwandamizi wa huduma za Mitaala na Utafiti Jacqueline Onyango alisema utaratibu wa mtaala wa elimu ya msingi (BECF) unategemea kile mototo anaweza kufanya wala sio anachoongea ama kuona.A�A�Bi. Onyango alisema hayo wakati wa jopo la majadiliano kuhusu mtaala wa elimu ya chekechea (ECDE). Mwenyekiti wa kitaifa ya KEPSHA Shem Ndolo na katibu David Mavuta walisema mtaala huo mpya ni mzuri na utekelezaji wake unapaswa kuhakikisha kwamba mafanikio ya mfumo wa elimu wa 8-4-4 hauvurugwi