Walimu Huko Nandi Wakashifu Mikataba Ya Kazi

Walimu huko Nandi wamesema mikataba ya kazi haitasaidia kuokoa kuzorota kwa viwango vya elimu katika kaunti hiyo.

Kulingana na katibu mkuu wa tawi la sehemu hiyo la chama cha kitaifa cha walimu, Boniface Tenai, serikali inapaswa kushughulikia tatizo la uhaba wa walimu katika kaunti hiyo kabla ya kufikiria kuhusu mikataba ya kazi kwa walimu ambao wana mzigo mkubwa wa kazi.

Tenai alisema mikataba ya kazi inaweza kuwa na manufaa ikiwa walimu wote wana kiwango cha kazi wanayoweza kushugulikia akiongeza kwamba katika baadhi ya shule baadhi ya walimu wanapaswa kuwa maradufu ya masomo wanayofundisha kwa wiki.

Aliishauri serikali kushughulikia mishahara duni ya walimu na wafikirie kuwapanisha vyeo walimu wakiokaa katika gredi moja kwa muda mrefu wa hadi miaka 10 .