Wakili Willie Kimani ,Josephat Mwenda, Joseph Muiruri Waandaliwa Ibaada Ya Wafu

Ibada ya pamoja ya wafu kwa wakili Willie Kimani,mteja wake Josephat Mwenda na dereva wa taxi Joseph Muiruri iliandaliwa leo asubuhi katika kanisa la Consolata, lililoko Westlands kabla ya marehemu Kimani kuzikwa jumamosi ijayo huko Kikuyu, kaunty ya Kiambu.Miili hiyo mitatu ilipatikana kwenye mto Ol Donyo Sabuk,Kilimambogo tarehe mosi mwezi julai.mauaji hayo yameshutumiwa na chama cha wanasheria nchini na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu huku wakiandamana kulalamikia mauaji hayo.maafisa wanne wa polisi wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayona wataendelea kuzuiliwa korokoroni hadi tarehe 18 mwezi huu wakati kesi yao itakapotajwa.Maafisa hao wanaozuiliwa ni sajini mkuu Fredrick Leliman, Sajini Leonard Mwangi, koplo Stephen Chebulet na konstebo Silvia Wanjiku.