Wakili Harun Ndubi ashtakiwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi

Wakili wa kutetea haki za binadamu,A�Harun Ndubi leo asubuhi alishtakiwa kwa kutatiza magari barabarani, kuendesha gari akiwa mlevi na kukaidi maagizo ya polisi. Ndubi ambaye alifikishwa mbele ya hakimu mkazi Electer Riany wa mahakama ya Milimani alikanusha mashtaka hayo na kuachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi 30,000 pesa taslimu. Ndubi alikamatwa jana usiku karibu na lango la D la ikulu ya Nairobi. Polisi wamesema Ndubi alikuwa akiendesha gari akiwa mlevi. Alikuwa akielekea nyumbani ambapo inadaiwa alisimama katika eneo hilo na kulala garini baada ya kulemewa na pombe. Alipelekwa katika kituo cha polisi cha Kileleshwa. Hata hivyo Ndubi anasisitiza kuwa alipewa dawa za kulevya.