Wakfu Wa Rockefeller Kusaidia Katika Ujenzi Wa Hospitali Ya Rufaa

Wakfu wa Rockefeller jana uliahidi kushirikiana na Mama wa taifa Margaret Kenyatta katika ujenzi wa hospitali ya rufaa iliyopendekezwa ya mpango waA� Beyond Zero itakayogharimu shilingi bilioni 2.2. Rais wa wakfu wa Rockefeller Dr Judith Seitz Rodin alimwambia mama wa taifa wakati alipomtembelea katika Ikulu kwamba wakfu huo utashirikiana na timu ya Beyond Zero kutekeleza mradi huo ili kuhakikisha unafaulu kama taasisi ya mafunzo, utafiti na matibabu kwa wagonjwa.A� Aliutaja mpango huo waBeyond Zero kuwa wakipekee na unaofaa kwa matokeo yanayoonekana.Mama wa taifa alisema amevutiwa na juhudi hizo na kufurahi kwa kukabidhi kliniki ya mwisho ya huduma za gari kwa kaunti ya Nairobi y.Halfa hiyo itafanyika katika Ikulu ya ,Nairobi, ambapo mama wa taifa pia atawashukuru wafadhili na wahisaniA� pamoja na waliounga mkono kusimama pamoja naye wakati safari ya miezi 33 ya kupanga na kuwasukusha klimiki za huduma za magari zipatazo 47 kwa kaunti zote nchini.Hospotali hiyo ya Beyond Zero ambayo mahala itakapojengwa jijini Nairobi itatambuliwa itakuwa ya kiwango cha hospitali ya rufaa.Hospitali hiyo itakayokuwa na vitanda 100-150 itapanuliwa katika ploti ya ekari 10.