Wakenya waungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya saratani duniani

Wakenya wameungana na walimwengu kuadhimisha siku ya saratani duniani. Siku hii imeadhimishwa huku ripoti mbili kuu zikiashiria kupungua kwa visa vya ugonjwa wa saratani na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo. Utafiti wa hivi punde unaashiria kuwa ugonjwa wa saratani unaweza kuzuiwa. Utafiti uliofanywa katika mataifaA� 71A� ,13 kati yao yakiwa barani Afrika unaashiria ongezeko la watu wanaopona kutokana na ugonjwa huo katika maeneo mengi ya dunia . Idadi kubwa zaidi ya wale waliopona kutokana na ugonjwa huo wanatoka katika mataifa tajiri .A� Dr Alfred Karagu, anayesimamia taasisi ya kitaifa kuhusu saraani katika wizara ya afya amesema ugonjwa huo unaweza kutibiwa.A� Dr. Karagu amesema hatua ya hazina ya kitaifa ya bima ya matibabu ya kufadhili matibabu ya ugonjwa huo itasaidia pakubwa kuboresha idadi ya watu wanaopona kutokana na ugonjwa huo hapa nchini. Amesema wameanza kushuhudia kupungua kwa mrundiko wa wagonjwa wa saratani katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta.