Wakenya Watakiwa Kujikinga Dhidi Ya Maambukizi Ya Kipindupindu

Katibu wa wizara ya afya Dr. Nicholas Muraguri amehimiza wakenya kujihadhari na chakula chochote wanachonunua huku kukiwa na ripoti za visa vya kipindupindu katika sehemu mbali mbali za Jamhuri. Hadi sasa inakadriwa kwamba watu 216 wamefariki na wengine wapatao elfu-13 kulazwa Hospitalini kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo. Ni kutokana na sababu hii ambapo wizara ya afya imeingilia kati kukabiliana na hali hiyo kwa kutambua jumla ya Kaunti 12 ambazo kwa sasa zimeripoti juu ya visa vya kipindi pindu. Aidha, wizara hiyo imesema KauntiA� 16 zimefanikiwa kupambana na ugonjwa huo. Dr. Muraguri alifafanua pia kwamba kuna baadhi ya kaunti ambazo zimeripoti juu ya ugonwja huo kwa mara ya kwanza, ilhali nyingine zinakabiliana na visa vya mara kwa mara. Alitaja kaunti za Wajir, Marsabit, Tharaka Nithi, Tana River, Meru, Busia na Nandi, ambazo zimeripoti mara ya kwanza juu ya ugonjwa wa kipindupindu. Dr. Muraguri alisema wagonjwa walioathiriwa zaidi ni wale wa umri wa miaka 46 kwenda juu, wakifuatiwa na wale wa umri wa miaka 5 hadi 15; Na kwamba visa vya ugonjwa huo ni vichache miongoni mwa watu wa umri wa miaka 36 hadiA� 45.