Wakenya wataka bei ya bidhaa muhimu ipunguzwe

Wakenya sasa wanataka serikali kuingilia kati kwa kupunguza gharama ya bidhaa nyingine muhimu ambazo bei yake imepanda kupita kiasi. Wito huo umetolewa saa chache baada ya serikali kuingilia kati na kupunguza gharama ya Unga wa Mahindi, ambapo pakiti moja ya kilo mbili sasa itauzwa kwa bei ya shilingi 90/=. Tangu mwanzo wa mwaka huu wa 2017 Wakenya wamelalamikia gharama ya juu ya bidhaa muhimu, huku waziri wa kilimo, Willy Bett, akisema kwamba muda unaokubaliwa kwa wamiliki wa kampuni za kibinafsi za kusaga unga, kuagiza mahindi bila kutozwa ushuru utamalizika tarehe 31 mwezi Julai mwaka huu. Hata hivyo, Wakenya sasa wanataka serikali kuchukua hatua za dharura za kuwanusuruA� kwa kupunguza ushuru unaotozwa bidhaa nyingine muhimu. Ijapo hatua ya kupunguza gharama ya Unga wa Mahindi imefurahiwa na wengi, mjadala juu ya Unga bado unaendelea,A� huku baadhi ya watu wakiibua maswali yaA� juu ya uhaba huo na kusema huenda ulisababishwa makusudi kutokana na sababu zisizoeleweka.