Wakenya wasubiri baraza jipya la mawaziri

Wakenya wanasubiri kwa hamu kubwa kuzinduliwa kwa baraza jipya la mawaziri, ambalo kulingana na Rais Uhuru Kenyatta, litatangazwa katika muda wa wiki chache zijazo. Rais yuko huru kudumisha mawaziri walioko sasa na kuwateuwa wengine wapya ikizingatiwa kwamba hakuna muda wowote kisheria ambao amewekewa kufanya hivyo.

Rais Kenyatta ambaye anahudumu kwa muhula wake wa pili na mwisho, anapojiandaa kustaafu mwaka 2022, yadaiwa ametambua tayari wale anaoamini wana ujuzi wa kutosha kutekeleza ahadi nne muhimu alizowapatia WaKenya; hususanA�Hali ya kujitegemea kwa chakula; Makaazi yenye gharama nafuu; Uimarishaji wa sekta ya utengenezaji bidhaa; Na huduma za matibabu zenye gharama nafuu kwa wakenya wote.

Huku kukiwa na uvumi kuhusu majina ya wale watakaojumuishwa kwenye baraza jipya la mawaziri, wandani wa karibu wa Rais Kenyatta kama vile David Murathe, ambaye ana ushawishi mkubwa katika utawala wa Jubilee, amedokeza kwamba huenda Rais akafikiria kudumisha wanachama waA�A�baraza la zamani la mawaziri.

Aidha, wanasiasa huenda wakanufaika pakubwa kutokana na uteuzi wa baraza jipya la mawiziri, hususan wale waliofanikisha kuchaguliwa tena kwa Rais Uhuru Kenyatta kwa muhula wa pili. Katiba ya Kenya inampa Rais uwezo wa kuteuwa baraza jipya la mawaziri wasiopungua 14 wala kuzidi A�22. Katika ujumbe wa kuukaribisha mwaka mpya, Rais Uhuru Kenyatta alidokeza kwamba yuko tayari kuzindua baraza jipya la Mawaziri kwa muhula wake wa pili ofisini, ijapo hakutaja tarehe kamili ya kufanya hivyo.