Matianga��i awashauri wakenya kupiga kura na kuondoka kwenye vituo vya kupigia kura

Kaimu waziri wa usalama wa kitaifa Dr Fred Matianga��i kwa mara nyingine amewashauri wakenya wapige kura na kuondoka kwenye vituo vya kupigia kuraA�wakati wa uchaguzi mkuu wa tarehe nane mwezi ujao. Dr Matianga��i pia amewataka vijana wadumishe amani wakati na baada ya siku ya uchaguzi huku akiwatahadharisha dhidi ya kutumiwa na wanasiasa ambao lengo lao ni kuzua uhasama miongoni mwa wakenya. Matiang’i alisema wakenyaA� wanapaswa kuchukulia uchaguzi huo mkuu kama uchaguzi mwengine na wasikubali kupotoshwa na wanasiasa. Taarifa hiyo ya waziri Matiangi inajiri zikisalia siku saba pekee kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Uchaguzi huo umebashiriwa kuwa mgumu na wanasiasa wamelazimika kutumia kila mbinu kuwarai wapiga kura kuwachagua .