Wakenya Wanaoishi Ng’ambo Hawatapiga Kura Katika Uchaguzi Mkuu Ujao

Muungano wa wakenya wanaoishi nga��ambo umedai kwamba haujashirikishwa kwenye shughuli ya usajili wa wapigaji kura licha ya agizo la mahakama ya juu. Mwenyekiti wa kamati ya sheria kuhusu upigaji kura wa wakenya wanaoishi, Nga��ambo Henry Ongeri amesema wakenya hao wamesikitishwa na mpango wa tume huru ya uchaguzi na mipaka wa kuanzisha usajili wa wapigaji kura tarehe-15 mwezi huu. Ongeri amesema tume hiyo imepuuza agizo la mahakama ya juu kuhusu kushirikishwa kwa wakenya walio ugenini kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017. Katika agizo lake la mwezi Mei mwaka uliopita mahakama hiyo iliagiza tume ya IEBC kuzindua mipango ya kuwawezesha wakenya wanaoishi Nga��ambo kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao. Tume hiyo iliagizwa kuwasilisha bungeni ripoti kuhusu maandalizi ya mpango huo lakini kufikia sasa haijatekeleza matayarisho yoyote kuhusu swala la usajili wa wakenya walio ugenini.