Wakenya walalamikia ghama ya juu ya bidhaa muhimu

Bei ya bidhaa muhimu inazidi kupanda, huku Maduka mengi kote nchini yakishuhudia uhaba wa Unga wa Mahindi na Sukari. Hayo yanajiri licha ya serikali kuamua hivi majuzi kuondolea ushuru bidhaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na mahindi yanayoagizwa kutoka ugenini,A� kwa madhumuni ya kupunguza bei ya bidhaa hiyo. Uchunguzi uliofanywa na shirika la KBC kwenye Maduka mbali mbali Jijini Nairobi, ulibaini kuwa pakiti ya kilo mbili za Unga wa Mahindi inauzwa kwa bei ya shilingi 165/=, Kilo moja ya Sukari shilingi 185/=, Ilhali Pakiti moja ya nusu a��Lita ya Maziwa inauzwa kwa bei ya shilingi 65/=.A� Wakenya wa tabaka mbali mbali sasa wanaitaka serikali kuchukua hatua madhubuti za kuwapunguzia mzigo huo wa mufumuko wa bei ya bidhaa muhimu.

Kwenye taarifa iliyochapishwa kwenye magazeti ya kila siku nchini, mamlaka ya kitaifa juu ya kilimo na chakula ilisema uhaba wa Sukari ulioko sasa umefikia tanni elfu-270, na kwamba hali hiyo imefanywa kuwa mbaya zaidi na uhaba ulioko wa bidhaa hiyo kwenye nchi zingine wanachama wa shirika la COMESA. Serikali inatarajiwa kuwasilisha mapendekezo mapya bungeni ili kushughulikia gharama ya maisha inayozidi kupanda, na ambayo imegeuka kuwa swala muhimu la Kampeini. Hapo Jana, taarifa kutoka Ikulu ilisema kwamba serikali itawasilisha bajeti ya ziada kwenye Bunge la kitaifa, ambalo litaanza vikao vyake leo, ili kuchunguza uwezekano wa kutenga fedha za kuwaondolea dhiki WaKenya. Na huku serikali inapojaribu kuingilia kati, Wamiliki wa kampuni za kusaga Unga wameonya kuhusu uwezekano wa kuongeza hata zaidi bei ya Unga wa mahindi katika muda wa miezi miwili ijayo, kwa kuzingatia gharama ya juu ya bidhaa hiyo. Wamiliki hao wa kampuni za kusaga Unga wanasema kwamba wamemaliza hifadhi za mahindi yenye gharama nafuu walizotengewa na halmashauri ya kitaifa ya nafaka na mazao, na hali mipango ya kuagiza bidhaa hiyo kutoka nchi jirani imefifia. Kwenye taarifa kwa vyumba vya habari, chama cha wamiliki wa kampuni za kusaga Unga kilisema hali hiyo imesababisha bei ya gunia moja la kilo 90 za Mahindi kupanda hadi shilingi 4,500