Wakenya waelezea hisia zao kuhusiana na uamuzi wa majaji wa mahakama kuu

Wakenya wameelezea hisia tofauti kuhusiana na ripoti za kina za uamuzi wa majaji wa mahakama ya juu kuhusiana na ile kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Urais. Baadhi yao wanasema sasa tume ya IEBC inafaa kurekebisha kasoro zote zilizokumba uchaguzi huo na kuandaa uchaguzi huru na wa haki huku wengine wakisema ripoti hizo za kina hazina maana yoyote kwasababu tayari mahakama hiyo imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa Urais wa tarehe nane mwezi Agosti. Katika kaunty ya Migori, wakazi walitoa maoni yao kuhusu hali ilivyo nchini kufuatia mashambulizi dhidi ya idara ya mahakama na madai ya ununuzi wa vitambulisho katika baadhi ya sehemu za magharibi mwa Kenya. Mwenyeiti wa kongamano la maaskofu huko Migori askofu Esau Jobando alishutumu kuingiliwa kwa idara ya mahakama. Wakili Ahmednasir Abdullahi amekosoa uamuzi kamili wa kesi hiyo uliofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa Urais. AbdullahiA�anadai kwambaA� mahakama hiyo inavurugha ushahidi. Wakili huyo pia anasema mahakama hiyo haikufaa kutoa uamuzi kama huo. Waklili mmoja wa Nairobi George Kegoro amesema endapo Maraga hatatatizwa kisiasa, huenda akaibuka kuwa jaji bora zaidi mkuu katika historia ya Kenya kwasababu hapendelei upande wowote. Mahakama hiyo imetoa ripoti za kina kuhusu uamuzi wake uliofutilia mbali ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.